11/07/2026
Habari njema kwa waendesha Bodaboda, madereva wa Tuktuk na Taxi wote wa Diani!
Kupitia uongozi wetu, tumefanikiwa kuweka ushirikiano utakaowezesha wanachama wetu kupata mafuta kwa bei ya discount saa 24 pale Chepechepe A&E Amoil Energies petro station.
Kuanzia kesho, fika kituoni hapo ujaze Petrol au Diesel kwa bei nafuu na uendelee kunufaika na fursa hii maalum.
Tunaendelea kujenga ushirikiano wenye manufaa kwa wanachama wetu. Asanteni kwa kuendelea kutuunga mkono na kushirikiana nasi.
Pamoja tuna nguvu, pamoja tunafaulu.